Radio sauti ya Istiqama kutoka Pemba iliasisiwa mwaka 2005 na Uongozi wa masjid Alkhali chini ya usimamizi wa Mwenyekiti wake sheikh Mohamed Suleimn Khalfan Tiwany.
Ni kituo cha kwanza cha radio kuanzishwa kisiwani Pemba na kimeanza rasmi kurusha matangazo tarehe 8/03/2010 hapo Misufini Chake Chake Pemba. Ilifunguliwa rasmi tarehe 10/7/2011 na Mufti mkuu wa Oman Samahat Sheikh Ahmed bin Hamed Al-Khalily na Naibu Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar
Kaaby katika Ukumbi wa ZSSF Chake Chake Pemba.
Sauti ya Istiqama kutokaPemba inapatikana katika masafa ya 107.1 FM na inasikika katika visiwa vya Unguja na Pemba, Dare es Salaam, Tanga pia inapatikana kupitia kwenye mtandao kwa kubofya Hapa.